Monday, 25 April 2016

Daraja la Kigamboni kusaidia kukuza Sekta ya Utalii

Daraja la Kigamboni kusaidia kukuza Sekta ya UtaliiSiku chache zimepita tangu daraja la Kisasa linalounganisha Kigamboni na jiji la kibiashara la Dar es salaam kukamilika na kuzinduliwa na Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufulbi.    

Daraja  hili lenye urefu wa mita 680 lilianzwa ujenzi  wake kuanzia  Mwaka 2012 mpaka kufikia 2016 limeweza kugharimu zaidi ya Dola  Million 140 ambapo inatarajiwa kuwa itakuwa ni chachu kwa  maendeleo na kukuza uchumi wa nchi Kupitia Kigamboni na Dar es Salaam.    

Jovago.com, kampuni inayojihusisha na kubook hoteli hapa Afrika imefafanua kuwa  kwa sasa Tanzania inaonyesha dalili nzuri za kukuza uchumi hasa katika masuala ya uchukuzi na usafirishaji , hali imekuwa ikiboreshwa kila mara.    

Andrea Guzzoni ambaye ni meneja mkazi wa Jovago hapa Tanzania alielezea kuwa Daraja la Kigamboni litaongeza wageni wengi wa kitalii katika mji huu, “Tumepoteza idadi nyingi ya watalii waliotamani kufikia hoteli za nje ya mji, ikifikia katika suala la usafiri ilikuwa ni shida kwa kipindi cha nyuma, tunaimani wageni wataongezeka wengi kwa kipindi hiki”    

“Daraja hili litaongeza kasi ya kukuza hoteli za kutalii kwani si watalii pekee waliokuwa na uwoga wa kuvuka boda kwa kutumia  Kivuko ila hata wawekezaji  pia walishindwa kujenga hoteli nyingi za kifahari”. Alifafanua.

0 comments :

Post a Comment