Friday, 8 April 2016

JovagoTanzania yaipongeza Zanzibar kwa kuimarisha utulivu katika kipindi cha Uchaguzi 2016

JovagoTanzania yaipongeza Zanzibar kwa kuimarisha utulivu katika kipindi cha Uchaguzi 2016Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Bw Andrea Guzzoni, Meneja Mkazi waJovago Tanzania alifafanua kuwa  pamoja na kuwa Uchaguzi wa Rais Zanzibar ulifanyika mara mbili lakini bado wananchi wamekuwa watulivu kiasi cha kufanya shughuli za kitalii kutoharibikika kama ilivyotegemewa.


Zanzibar ni mji wa Utalii, Kama kungekuwa na vurugu za aina yeyote hii ingeharibu shughuli za kiserikali na soko la mji huu kwa kiasi kikubwa”.  Aliongezea.


Kwa Upande wake, Lilian Kisasa, Meneja Mawasiliano wa JovagoTanzania, aliongezea kwa kusema kuwa watalii wengi waliokuwa wanaingia Zanzibar na kubook hoteli ni watanzania wenyewe,  ambapo  idadi ndogo ya watalii kutoka nje ilipungua kwa 5%  tu, Hata hivyo haikuweza kuathiri soko la utalii kwa kiwango kikubwa.


Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) iliweza kutangaza marudio ya uchaguzi visiwani humo baada ya matokeo  yaliyopita kufutwa, ambapo, Dr. Ali Mohamed Shein alitangazwa rasmi kuwa mshindi wa marudio ya uchaguzi wa urais Zanzibar.


Aidha serikali imeombwa kuhimiza hasa utalii wa ndani kwani bado Watanzani wamekuwa wako nyuma katika kutembelea hifadhi zao wenyewe ambapo ,hatua hii ikiimarika itaweza kuongeza pato la taifa kwa asilimia kubwa.


Kuhusu Jovago

Jovago.com, tovuti inayorahisisha huduma za ku book hoteli kupitia mitandaoni. Ofisi kuu hapa Africa zipo Lagos (Nigeria), Nairobi kenya, na  Dakar (Senegal). Jovago.com imegunduliwa  na kampuni ya Africa Internet Group (AIG) chini ya udhamini wa MTN, AXA na Millicom Read more....

0 comments :

Post a Comment